THE AMBASSADOR OF SWEDEN TO TANZANIA HAS VISITED THE TEND TEN TREES PROJECT!

On Tuesday 23rd of April 2024, the Ambassador of Sweden to Tanzania, Her Excellency Charlotta Ozaki Macias, visited us! She was invited by Rt. Rev. Dr. Stephen Munga to visit the Tend Ten Trees project here in Maramba that was launched in 2022 by the Initiative for Peace and Reconciliation (IPR).

BALOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA APONGEZA MRADI WA TEND TEN TREES MARAMBA

Tanga Anglican Media

Jamii nchini imeaswa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kuendelea kuotesha miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaikumba dunia katika nyanja tofauti ikiwemo athari za hali ya hewa.

Wito huo ulitolewa Aprili 23, 2024 na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Maramba mkoani Tanga waliojitokeza kumlaki kisha kufanya Ibada katika Kanisa Anglikana Kujiliwa na Bwana Maramba Msumbiji.

Shemasi Michael Mbwana wa Kanisa Anglikana Kujiliwa na Bwana Maramba Msumbiji akiongoza ibada fupi na kumkaribisha Balozi wa Sweden nchini Tanzania alisema, uhifadhi wa mazingira ni agizo la Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.

“Katika Injili kama alivyoiandika Luka Mt. 13:6-9 ipo habari ya mtu aliyekuwa na mti wa mtini katika shamba lake la mizabibu. Alipoona mtini hauzai matunda alitaka kuukata. Lakini mtunza shamba aliomba muda ili aweze kuuhudumia mtini ule na kuweka samadi ili uzae matunda,” alisema Shemasi Michael Mbwana.

Ujio wa Mhe. Charlotta Ozaki Macias, Balozi wa Sweden nchini Tanzania katika Kata ya Maramba ni matokeo ya mwaliko wa Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dr. Stephen Munga, kupitia Asasi iliyozinduliwa mwaka 2022 iitwayo Initiative for Peace and Reconciliation yenye lengo la kuhamasisha jamii kuishi katika hali ya amani na upatanisho.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Maramba na baadhi kutoka kata jirani waliojitokeza katika Kanisa Anglikana Kujiliwa na Bwana Maramba Msumbiji, Askofu Munga alisema ziara ya Balozi huyo ililenga kuona na kukagua shughuli za kijamii zinazoendelea chini ya Initiative for Peace and Reconciliation.

Aidha alisema lengo la Asasi hiyo ni kugusa maisha ya wananchi bila kujali itikadi za dini ili kutoa hamasa ya kuishi katika misingi ya amani na upatanisho, ikiwemo kuwapa wakulima na wafugaji elimu ya kufanya shughuli zao bila uvunjifu wa amani.

“Tangu mwanzo tulieleza kuwa Asasi yetu itaendelea kusimama katika lengo la kusaidia jamii kuishi katika msingi wa amani na upatanisho. Tumeanza na Maramba lakini tutafika na maeneo mengine. Sisi tunasaidia watu bila kujali dini zao,” alisema Askofu Munga.

Mchungaji Anneth Munga, Mkurugenzi wa Miradi katika IPR alisema Asasi hiyo inaendesha Mradi wa kupanda miti, Tend Ten Trees, katika kata ya Maramba ikimaanisha kila mshiriki anapanda na kutunza jumla ya miti kumi. Hadi sasa miti 2,280 imeoteshwa.

“Mradi huu unahusisha familia kupitia wanawake kupanda miti kuzunguka maeneo wanayoishi. Kila mwanamke anapewa miche kumi ya miti tofauti ya matunda na pia anapewa kiasi kidogo cha fedha ili kurahisisha utunzaji wa miti hiyo kumwagilia kipindi kisicho na mvua. Fedha hiyo pia inatumika kununua na kupanda miche mipya endapo baadhi itakufa kwa kuliwa na wadudu waharibifu,” alisema Mchungaji Anneth Munga.

Aidha Mchungaji Anneth akiambatana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe, Charlotta Ozaki Macias na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Asasi ya Initiative for Peace and Reconciliation walitembelea maeneo ya baadhi ya familia zilizopanda miti chini ya Mradi wa Tend Ten Trees na kuona maendeleo yake huku Balozi huyo akipongeza jitihada hizo.

Clement Shehiza, Mratibu wa Mradi wa Tend Ten Trees unaoendelea kupitia Asasi ya Initiative for Peace and Reconciliation alisema ziara ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania inaithibitishia dunia kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili umekuwa na faida kwa wananchi.

“Tunayo furaha kubwa ya ujio wa Balozi anayewakilisha nchi ya Sweden hapa kwetu Tanzania. Wananchi wa Maramba tunaamini ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi mbili umekuwa na faida kwetu,” alisema Mratibu huyo.

“Nchi ya Sweden ni miongoni mwa nchi chache duniani inayounga mkono jitihada za kupambana na uharibifu wa mazingira. Tumetambua umuhimu huu nasi tumeendelea kupanda miti,” alisema Clement Shehiza, Mratibu wa Mradi.

Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wa kupanda miti akiwemo Bi. Selestina Tunguli na Rose Mwinyimbwana walisema mradi huo umekuwa na tija kwao kwa kuwa licha ya kuhifadhi mazingira miti hiyo ya matunda itawanufaisha kiuchumi baada ya mavuno.

“Mradi huu tumeupokea vizuri, tunawashukuru waliouanzisha ili kuisaidia jamii kujikwamua kiuchumi na kutunza mazingira. Tunapewa miche kumi ya miti tofauti ya matunda ili tukaoteshe katika mazingira yetu na kuitunza.”

“Wananchi tunashirikishwa bila kujali dini zetu. Tulianza awamu ya kwanza mwaka 2022 na sasa tunaendelea awamu ya sita na saba. Idadi ya washiriki wanawake imeendelea kuongezeka baada ya kutambua thamani ya mradi huu,” walieleza wananchi hao.

Licha ya kushiriki na kujionea mafanikio ya mradi huo, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe, Charlotta Ozaki Macias alitumia nafasi hiyo kugawa miche ya miti ya matunda kwa washiriki wapya awamu ya sita na saba ambao wameenda kuifanyia kazi.

Sweden’s Ambassador to Tanzania to visit Maramba

On Tuesday 23rd of April 2024, the Swedish Ambassador to Tanzania, H.E. Charlotta Ozaki Macias, will visit Maramba. It will be the first time for Maramba to be visited by an ambassador from a foreign country. H.E. Macias has been invited to Maramba by the founder of the Initiative for Peace and Reconciliation (IPR), Rt. Rev. Dr. Stephen Munga. The Ambassador will get to know the Tend Ten Trees project which is conducted by the IPR.

Sweden is a country that is deeply engaged in climate change mitigation. It is therefore fitting that the ambassador of that country gets an opportunity to see how a truly Tanzanian project engages people at grassroot level in nature preservation.

Karibu sana, Mhe. Charlotta Ozaki Macias! You are warmly welcome to Maramba!

Pastor Bill Erat in memory

PASTOR BILL ERAT who died in November 2023 is fondly remembered for the support he and his congregation in Glenside, USA, gave to the Tend Ten Trees. In November 2023 we planted 5 mango trees in Pastor Bill’s memory…

28 YOUNG STEWARDS OF LIFE!

Energetic pupils of the 2024/2025 Confirmation class at the Anglican Church in Maramba are queuing to receive tree plants. From the Tend Ten Trees (TTT) programme, each of these children has been given a mango tree to plant and tend. Through action they learn that being God’s steward means being actively responsible to preserve the life God has given us. Planting fruit trees and caring for them is one way of being a steward of life.

The 28 confirmation pupils who are now tending their own mango trees at their homes are 11 girls and 17 boys. The girls are Anjelina, Anna, Anneth, Esther, Jestina, Marystina, Patricia, Philomena, Rachel, Saumu and Salome. The boys are Aidano, Charles, Daniel, Daudi, David, Dennis, Elias, Emmanuel, Julius, Michael, Nathaniel, Omari, Samwel, Yakobo, Yohana, William and Wilson.

Instagram